Ecclesiastes 12:3-6

3 asiku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka,
nao watu wenye nguvu watakapojiinamisha,
wakati wasagao watakapokoma kwa sababu ya uchache,
nao wachunguliao madirishani kutiwa giza;
4 bwakati milango ya kuingia barabarani itakapofungwa
na sauti ya kusaga kufifia;
wakati watu wataamshwa kwa sauti ya ndege,
lakini nyimbo zao zote zikififia;
5 cwakati watu watakapoogopa kilichoinuka juu
na hatari zitakazokuwepo barabarani;
wakati mlozi utakapochanua maua
na panzi kujikokota
nawe usiwe na shauku ya kitu chochote.
Ndipo mwanadamu aiendea nyumba yake ya milele
nao waombolezaji wakizunguka barabarani.

6Mkumbuke Muumba wako: kabla haijakatika kamba ya fedha,
au bakuli la dhahabu halijavunjika;
kabla mtungi kuvunjika kwenye chemchemi,
au gurudumu kuvunjika kisimani,
Copyright information for SwhNEN